Kufuatia kuijiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni Maulid Mtulia, Mgombea Ubunge wa Jimbo hilo ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Salum Mwalimu amefunguka kuwa hakuna wa kumkataza kuongea jambo lolote lenye tija kwa watu wake wa kinondoni mara achuguliwapo kuliongoza jimbo hilo.

Ameongezea kuwa yupo tayari kuwa mwendawazimu kwa kuwapigania wananchi wa jimbo hilo akiwa Bungeni.

Salum Mwalim ameeleza hayo ikiwa imepita siku moja toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuruhusu kuanza kwa kampeni rasmi za uchaguzi mdogo katika majimbo mawili ambayo ni Kinondoni na Siha.

“Nakwenda Bungeni kulia na kuwa mwendawazimu kwa mahitaji ya watu wa Kinondoni, hakuna wa kunikataza kuongea jambo lolote ambalo litakuwa lina tija kwa watu wangu. Nitahakikisha narudisha heshima ya kinondoni”, alisema Salum Mwalim.

Uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni unatarajiwa kufanyika mwezi ujao (Februari 17, 2018) ili kuweza kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kwa tiketi ya chama cha wananchi (CUF), Maulid Mtulia aliyejiuzulu kiti na uanachama kwa chama hicho na nafasi zote za uongozi alizokuwa nazo hapo awali.

 

Alichoandika Aunt Ezekiel chaibua hisia za wengi mtandaoni
Ziara ya Majaliwa yang'oa kigogo Mara