Wananchi wa eneo la Sogea, Wilaya ya Mjini Unguja wamemkabidhi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni orodha ya majina ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya Visiwani Zanzibar.
 
Wananchi hao wamekabidhi orodha hiyo baada ya Masauni kuwataka waorodheshe majina ya watu wanao wafahamu wakituhumiwa kujihusisha na biashara hiyo ambayo imekuwa ikiharibu nguvu kazi ya Taifa na kusababisha kuwepo kwa matukio ya uhalifu katika sehemu mbalimbali Visiwani humo.
 
Awali wakiwasilisha kero zao kwa nyakati tofauti tofauti wananchi hao waliiomba serikali kudhibiti biashara hiyo ya dawa za kulevya kwani imekua ikishamiri kwa kasi Visiwani humo na wakishangaa ukimya wa mamlaka husika kuacha biashara hiyo kwani ikizidi inaweza kuleta madhara katika jamii.
 
Akizungumza katika Mkutano huo wa hadhara, Masauni amewaahidi wananchi hao kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na wauzaji wa dawa za kulevya huku akitoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata watu wote wanao tuhumiwa na uchunguzi uanze mara moja.
 
“Kama Taifa hatutakubari kuwa na vijana ambao hawana faida katika jamii, vijana ni nguvu kazi ya Taifa, tutahakikisha majina yaliyoletwa hapa tunayafanyia kazi na natoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa hao wanakamatwa na nitahitaji ripoti hiyo ndani ya wiki mbili,”amesema Masauni
 
  • Anyongwa kwa sweta la mumewe
 
  • Mbatia amshtaki Warioba kwa JPM
 
  • Unatafuta ajira? hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako
 
Hata hivyo, Kamishna Msaidizi, Saleh Mohamed Saleh, aliwaomba wananchi kuzifikisha taarifa za uhalifu katika vituo vya Jeshi la Polisi au Serikali ya Mtaa ili hatua ziwe zinachukuliwa kuweza kudhibiti uhalifu katika maeneo yao.

Majaliwa achukizwa wanafunzi 72 kupewa ujauzito Nyang’hwale, atoa maagizo mazito
Hatma ya kesi ya Mbowe, Matiko utata, yapigwa kalenda tena