Rais dkt. John Magufuli ameagiza wakuu wa usalama wilayani Arumeru waondolewe katika nafasi zao akiwepo, OCD, OCCID na afisa usalama.

Katika hotuba yake wakati wa kuwaapisha Wakuu wa Mikoa, ametoa maagizo hayo baada ya Kaimu Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti dawa za kulevya kwenda Meru na kukamata magunia ya bangi.

Magufuli ametoa maagizo hayo huku akishangaa viongozi hao wa Usalama walikuwa wakifanya nini wasikamate bangi hizo.

“Haiwezekani utoke wewe (Kamishna Jenerali wa Mamlaka), James Kaji Dodoma hapa Makao Makuu au Dar es Salaam hapa ndio ukazione bangi wakati kule wakati kuna viongozi wapo kule kuna OCD wa wilaya ya Arumeru, IGP nataka Mkuu wa polisi Arumeru aondolewe, Afisa usalama” Amesema Magufuli.

Pamoja na hilo Rais ametambua utendaji wa Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Dawa za Kulevya, James Wilbert Kaji na kumteua kuwa kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo.

Rais Magufuli amesema anaamini zaidi utendaji na kuwateua watu kutokana na utendajio kazi wao

Watakaoandamana "77 Nyeupe" kushughulikiwa
DC Sabaya aingilia kati viongozi kuwapaka wanawake 'upupu' sehemu za siri

Comments

comments