Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar (ZMA), imewataka kampuni ya Azam Marine na Fast Ferries inayofanya safari zake za majini Dar es salaam na Zanzibar kusitisha safari hizo mpaka pale watakapo arifiwa tena na mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Hali ya Hewa ya Zanzibar safari hizo zimesitishwa kuanzia leo Oktoba 23, 2018 kutokana na hali ya hewa kuwa si shwari kwani kumekuwa na mvumo wa upepo mkali hali inayohatarisha vyombo vya usafiri wa majini.

Mamlaka imesema safari hizo zitarejeshwa tena mpaka hali ya hewa ya baharini itakapotulia.

Aidha, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) jana iliarifu kuwa leo kutakuwa na upepo wa Pwani unaotarajiwa kuvuma kutoka Kusini kwa kasi ya Km 50 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini, na kwa kasi ya Km 60 kwa saa kwa Pwani ya Kusini huku hali ya hewa ya bahari ikitarajiwa kuwa na mawimbi makubwa.

Hata hivyo kwa siku ya leo katika baadhi ya maeneo kumekuwa na upepo mkali unaovuma kwa kasi kubwa hali inayoashiria huko baharini si shwari, hivyo abiria ni vyema wakatumia usafiri wa anga kama safari zao ni za muhimu sana kuliko kukiuka agizo la mamalaka ya hali hewa.

Kufahamu zaidi juu ya sitisho hilo ni vyema kuwasiliana na Azam Marine na Kilimanjaro au kutembelea ofisi zao.

Video: NECTA yatangaza matokeo ya Darasa la Saba
Video: Muonekano wa ndani ya ndege ya kifahari zaidi duniani