Nchi ya Afrika kusini imekua ya kwanza kutangaza hadharani nia ya kuomba nafasi ya kuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali wa michuano ya ngazi ya vilabu barani Afrika( Ligi ya mabingwa barani Afrika, kombe la Shirikisho Afrika).

Juma lililopita CAF walifungua milango kwa nchi wanachama kuwasilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa mchezo wa fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na kombe la shirikisho, ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo, kufuatia mabadiliko yaliyopitshwa chini ya utawala wa Rais Ahmed Ahmad.

CAF wamefanya mabadiliko hayo ili kuondoa mfumo wa zamani, ambao ulitoa nafasi kwa michezo ya michuano hiyo kuchezwa nyumbani na ugenini, jambo ambalo lilikua linazigharama baadhi ya klabu zilizofia kwenye hatua ya fainali.

Mtendaji mkuu wa shirikisho la soka Afrika kusini (SAFA) Gay Mokoena, amesema kabla ya kutangaza nia hiyo hadharani, tayari wameshafanya mazungumzo na uongozi wa Majiji na Manispaa ambayo yanamiliki viwanja vyenye hadhi ya kuhodhi moja ya michezo ya fainali ya ngazi ya vilabu barani Afrika.

Mokoena amesema wanaamini Afrika kusini ina kila vigezo vya kushinda mchakato wa kumsaka mwenyeji wa michezo hiyo ya fainali, na watawasilisha maombi yao haraka iwezekanavyo.

Casillas atia nia urais RFEF

CAF imetoa nafasi ya kupokea maombi kutoka kwa nchi wanachama hadi Februari 20, na baada ya hapo mpango wa kukamilisha mchakato wa kutangazwa washindi utafanyika.

Mchezo wa fainali wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAF Champions League) umepangwa kufanyika Mei 29, huku mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup) ukitarajiwa kuunguruma Mei 24.

Ndayiragije: Nitaiandaa vyema Taifa Stars
Abiria waliokwama melini kwa kuvamiwa na Corona waanza kuokolewa