Polisi katika Wilaya ya Apac, nchini Uganda wameanza uchunguzi dhidi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 19 anayedaiwa kumzika mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miezi miwili akiwa hai hapo jana.

Vyombo vya Usalama Wilayani humo vimethibitisha kutokea kwa tukio hilo na vinaendelea na uchunguzi huku mtuhumiwa akiwa Rumande.

Taarifa zinaeleza kuwa mwanamke huyo alifikia hatua hiyo baada ya wazazi wake kumnyima chakula wakidai kuwa amezaa mtoto haramu.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa mtuhumiwa alitoweka na mtoto wake nyumbani kwao kwa muda wa siku tatu na aliporudi Jumatatu hakuwa amerudi naye na kusema kuwa amemzika baada ya kutengwa na familia.

Aidha, Kumekuwa na tabia ya familia kuwatenga watu wanaojifungua watoto wenye ulemavu,  hali inayopelekea wazazi kujisikia upweke na kuona wenye mkosi na balaa na wengine kuwapelekea kuchukua hatua kama hiyo.

 

Nugaz: Shabiki wa yanga asiyenunua jezi orijino, anahujumu timu, ''Ndio maana hatulipi madeni''
Serikali yakiri kutokuwa na takwimu za magonjwa yasiyoambukizwa

Comments

comments