Uhaba wa maji na wananchi kutozingatia kanuni za usafi wa mazingira ni moja ya sababu inayopelekea kushamiri kwa ugonjwa wa trakoma kwenye baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Singida.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Singida Dkt. Ernest Mugetta katika kikao cha tathmini ya robo mwaka kilichowakutanisha wadau mbalilmbali wanaojihusisha kukabiliana na ugonjwa wa huo wa Trakoma ndani ya Halmashauri za wilaya ya Manyoni na Ikungi.

Amesema pamoja na dalili za mafanikio zilizopo katika kupambana na kudhibiti ugonjwa huo bado jitihada za ziada zinahitajika kwa kila mdau kushiki kutoa maoni yake juu ya nini kifanyike ili kuweza kutokomeza ugonjwa huo.

”Bado tunaendelea kutoa elimu hasa kwenye kuzingatia masuala ya usafi wa macho, maji na kunawa uso vizuri kwani hivi ni vitu ambavyo tunaendelea kuvisisitiza sana kwenye jamii ili kupunguza ugonjwa huo wa macho uitwao trakoma unaoathiri maeneo yenye uhaba wa maji,” amebainisha Dkt. Mugetta.

Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia wanasa Takukuru

Aidha Mugetta ameongeza kuwa serikali kwa kushirikiana na Shirika lisilo la kiserikali la Helen Keller International wameendelea kutoa huduma za afya ya macho kwa mafanikio ndani ya Halmashauri za Manyoni na Itigi na kuhamasisha umma juu ya kuchukua tahadhari.

Amefafanua kuwa suala la uchukuaji wa tahadhari ni muhimu kwani itasaidia kuepukana na ugonjwa huo na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kuzingatia usafi wa macho wakati wote kwani trakoma huwapata watu wote wenye umri wa miaka 15 na kuendelea.

Awali afisa mradi wa Trakoma kutoka Shirika la Helen Keller International Athuman Tawakal amesema tatizo la ugonjwa huo lipo kwa mda mrefu lakini limekuwa likipungua kwa kiasi chake.

Lugola awaonya wanaosafirisha wahamiaji haramu

Amesema kwasasa juhudi iliyopo ni kuhamasisha jamii kuondokana na visababishi vyote vinavyoweza kusababisha ugonjwa huo ikiwemo kuzingatia suala la usafi wa mazingira, upatikanaji wa maji ya kutosha ndani ya jamii, ujenzi wa vyoo bora na kutoa matibabu kwa wale wote ambao wameathirika dhidi ya ugonjwa huo

Trakoma ni ugonjwa unaoathiri macho ambapo kope huingia ndani na kugusa jicho hatimaye matokeo ya hali hiyo huweza kumsababishia mtu kutoona vizuri au kupatwa na upofu.

Wanaume milioni 4,456,511 wafanyiwa tohara nchini
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Novemba 16, 2019