Wizara ya afya nchini Rwanda imetangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya Corona miongoni mwao akiwa ni mtoto wa miezi 10, maambukizi hayo yanaifanya rwanda kuwa na idadi ya visa vya maambukizi ya Corona kufikia 17, immelezwa kuwa waliopatikana na maambukizi hayo walitoka katika nchi za ng’ambo.

Hata hivyo wizara ya afya imewataja watu hao sita kuwa ni mwanamke mfaransa (30) na mtoto wake wa miezi 10 ambaye pia amepatikana na maambukizi ya virusi hivyo akiwa na mtoto mdogo zaidi aliyewahi kupatikana na Covid 19.

Mwingine ni myarwanda miaka (32) aliyefika nchini Rwanda akitokea wegeze Dubai, na mwananume kutoka Sweeden aliyefika Rwanda March 3,2020 na dalili za Corona zilianza kuonekana  March 18, 2020, mwanaume Myarwanda mwenye umri wa miaka 32 ambaye  alionesha dalili za Corona March 18, 2020 huku mwanaume mwingine mwenye umri wa miaka 24 aliyefika Rwanda March 19, 2020 kutokea India.

Kwa mujibu wa Wizara ya afya nchini humo wagonjwa wote wametengwa na wanaendelea kupata matibabu hata hivyo wizara Inawaomba watu wote waliofika nchini Rwanda katika kipindi cha siku 14 zilizopita kujitenga binafsi kwa siku 14 na kufuata maagizo yaliyotolewa juu ya virusi vya corona.

Waziri wa Afya nchini humo Anastase Shyaka alitangaza kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini vimeahirishwa na wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.

Shirikisho la Soka la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.

Watakaoongeza bei vifaa kinga vya Corona kuchukuliwa hatua za kisheria
Nugaz aitaka Simba SC ASFC

Comments

comments