Urusi imesema kuwa itaendelea na mpango wake wa kuunda makombora yaliyopigwa marufuku chini ya mkataba wa vita baridi ikiwa Marekani itajiondoa katika mkataba unaodhibiti silaha hizo,

Tamko hilo limetolewa na rais wa nchi hiyo, Vladmir Putin ambapo amesema kuwa shirika la kujihami kwa mataifa ya magharibi Nato, kuilaumu Urusi kwa kukiuka mkataba wa makubaliano kudhibiti uundaji wa makombora ya masafa ya kadri (INF).

Aidha, makubaliano hayo yaliyotiwa saini mwaka 1987 kati ya Marekani na USSR, yalipiga marufuku mataifa hayo yote mawili dhidi ya kuunda makombora ya masafa mafupi na yale ya kadri.

Rais Putin amesema kuwa tuhuma za Nato dhidi ya taifa lake ni kisingizio cha Marekani kujiondoa katika mkataba huo.

“Sasa inaonekana kuwa washirika wetu Marekani wanahisi kwamba mambo yamebadilika sana kiasi cha kuwa wanaonelea ni lazima wao pia wawe na silaha, sisi pia tutafuata mkondo huo huo,”amesema Putin

Hata hivyo, rais wa Marekani, Donald Trump siku za hivi karibuni aligusia kuwa taifa hilo huenda likajiondoa katika mkataba huo kutokana na mienendo ya Urusi.

Majaliwa afungua kiwanja kipya cha Baseball jijini Dar
‘Wajanja’ wapiga asilimia 60 ya umeme wa Serikali

Comments

comments