Mwenyekiti Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMA), Hashim Rungwe Spunda amefunguka na kusema hakuna tatizo Lowassa kukutana na Rais Magufuli lakini amedai kuwa ni lazima tujue watu hao walipokutana Ikulu walizungumza nini kwani sasa imebaki siri yao.

Ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na moja ya chombo cha habari nchini na kudai kuwa Lowassa hapaswi kulaumiwa ila tu ni lazima aweke bayana kile ambacho alikaaa na kuzungumza na Rais Dkt. Magufuli ili Watanzania wajue jambo hilo lina maslahi wapi.

“Hatujui walichozungumza maana mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambaye anafahamu watu hao wamezungumza nini, Rais Magufuli mwenyewe hakusema nini wamezungumza na Lowassa hata Lowassa mwenyewe hajasema mpaka sasa nini amezungumza na Rais Magufuli hivyo imebaki ni siri yao, sasa hii siri yao lazima tuitafute na kuijua baadaye kama ina faidi kwa upande wetu au ina faida upande ule moja kwa moja,”amesema Rungwe

Hata hivyo, Rungwe ameongeza kuwa kwa watu ambao wanaona bado Serikali ya awamu ya tano haijibu hoja na kutatua matatizo ya wananchi wanapaswa kuendelea kupiga kelele na wale ambao wanaona Rais Dkt. Magufuli ametekeleza mambo nao waendelee kumuunga mkono.

Nyani kumpeleka jela Chris Brown
CCM yaibuka kidedea uchaguzi mdogo