Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imepitia mwenendo wa matukio ya Ligi na kufanya maamuzi mbalimbali ikiwemo utoaji adhabu kwa wahusika.

Katika kikao hicho cha February 03, 2020, Kamati imeridhia kumfungia miaka mitatu Mwamuzi msadizi namba mbili wa mchezo namba 150: kati ya Simba SC (3-2) Namungo FC Kassim Safisha kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea (offside) katika mechi hiyo na kwamba adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39(1) (a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.

Wakati huo huo Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi namba 157 iliyochezwa Januari 30, 2020 kati ya Azam FC (1-1) Mtibwa FC kwenye Uwanja wa Taifa.

Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya Makamishina kutokana na kutoa taarifa yenye mapungufu huku adhabu hiyo ikitafsiriwa kulingana na Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina wa mchezo.

Katika mechi namba 75A kati ya Friend Rangers (0-1) Dodoma FC, Kiongozi wa Klabu ya Friends Rangers Heri Chibakasa amepelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) kwa kosa la kupigana na mashabiki wa timu pinzani.

Aidha TPLB imetoa adhabu kwa Mwamuzi Salum Mkole ambaye amefungiwa miezi mitatu kwa kosa la kuonyesha udhaifu katika usahihi wa kutoa kadi katika mechi namba 29A iliyochezwa Januari 31, 2020 kati ya Dar City Fc (1)-(0) African Sports, katika dimba la Uhuru.

Wakala afikiria kumrudisha Jorginho kwa Maurizio Sarri
Eric Abidal: Tulisitisha kumsajili Aubameyang