Baadhi ya wazazi wa kike mkoa wa Rukwa wameanza kuwapa mabinti zao wenye umri mdogo baada ya kubalehe dawa za kupanga uzazi ili kuwaepusha na mimba za utotoni wakiwa shuleni.

Akizungumza katika kikao cha kamati ya ulinzi na usalama wa watoto na wanawake, mmoja wa wazazi Annakleda Nkale (64) amekiri kuwa wapo wazazi wakike ambao wanawapatia dawa mabinti zao ili kuwakinga wasipate ujauzito wakiwa shuleni.

“Katika hili suala zima la kukabiliana na changamoto ya mimba za utotoni, baadhi ya wazazi wa kike wanafanya hivyo ili watoto wao wakike wasipate ujauzito wakiwa shuleni, namfahamu mzazi ambaye binti yake anasoma kidato cha tatu alinieleza wazi kuwa binti yake alianza kutumia dawa za mpango wa uzazi mara tu alipojiunga kidato cha tatu” alifafanua Nkale.

Baadhi ya wanawake wengine ambao walihudhuria kikao hicho pia walikiri kufanya hivyo kutokana na kiwango cha kutisha cha mimba za utotoni mkoani humo.

Wakitaja baadhi ya sabubu zinazopelekea idadi ya wanafunzi kupata mimba mkoni humo kwa kasi wamesema ni uwepo wa maeneo hatarishi kama, minada, masoko, magulio, kumbi za starehe na burudani hususani usiku.

Kikao hicho kiliwashirikisha wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama wa watoto na wanawake na kupinga mimba za utotoni kutoka kata nne za Namanyere, Nkandasi, Nkomolo na chala zilizopo katika wilaya ya Nkasi chini ya uratibu wa asasi ya GCDE kwa ufadhili wa asasi ya Foundation for civil society (FCS).

Waasi watumia ndege zisizo na rubani kushambulia wanajeshi Yemen
Wanawake U -20 washusha kipigo Uganda