Matumaini ya kukata rufaa yamefifia baada ya Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi hayo yaliyowakilishwa na Wakili wa aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni.

Bageni aliiomba Mahakama ya Rufaa iridhie kumfutia adhabu ya kunyongwa kwa kosa la mauaji ya Wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

Aidha, uamuzi huo wa Mahakama, umehitimisha kesi hiyo iliyodumu kwa miaka 13 tangu washtakiwa walipopandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza mwaka 2006.

Tangu wakati huo washtakiwa walikuwa wakipungua katika kila hatua ya kesi, hadi kubakia ndugu Christopher Bageni peke yake.

Washtakiwa wengine waliowahi kujumuishwa katika kesi hiyo kabla ya kuachiwa huru ni aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es salaam (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi, Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP), Ahmed Makelle, na Askari wa Kituo cha Polisi Oysterbay, Rajabu Bakari.

Wakurugenzi 40 matatani, 'Jielezeni kwanini tusiwachukulie hatua'
Kitendawili cha kesi ya Lissu kuanza leo