Askari wa Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani, wametakiwa kufanya kazi zao kwa weledi na kuacha kuomba na kupokea rushwa.
 
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Wankyo Nyigesa wakati akizungumza na askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Kibaha mkoa wa Pwani.
 
Amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko kwa baadhi ya askari wa usalama barabarani kujihusisha na vitendo vya kuomba na kupokea rushwa jambo ambalo limekuwa likichafua taswira ya Jeshi la Polisi.
 
“Katika kipindi cha uongozi wangu nitakuwa mkali na sitosita kuchukua hatua kwa askari yeyote atakayebainika kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa madereva,”amesema Wankyo
 
Aidha Wankyo, amewataka askari hao kuzingatia utoaji wa huduma bora kwa wateja wanaowahudumia kila siku na kuacha vitendo vya malumbano na majibu yasiyozingatia utu kwa wale wanaowahudumia katika barabara.
 
Hata hivyo, amewaasa madereva wanaoingia ndani ya mkoa wa Pwani kuzingatia sheria za usalama barabarani na wale watakaokaidi kutii sheria hizo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
 
  • Wananchi Wanging’ombe waanza ujenzi wa kituo cha afya
 
  • CCM Njombe wamng’ata sikio mwenyekiti wa chama hicho Iringa
 
  • BOT yafunga benki nyingine

Nairobi: Shuhuda aeleza alivyowaona magaidi wakiitembelea hoteli mara 4
Wananchi Wanging'ombe waanza ujenzi wa kituo cha afya