The Goddess Rapper kwa lugha ya kigeni, Rosa Ree amesema kuwa na mtoto na kuanzisha familia ni lengo lake kuu katika maisha, na itampa furaha akiifanikisha.

Rapa huyo wa ‘Banjuka’ ameeleza kuwa kama mwanamke, anatamani kuwa chanzo cha kumpa uhai binadamu na kumfanya aishi na kwamba huo ndio mpango wa Mungu ambao atafarijika akiufikia.

“Yeah, napenda sana, na lengo langu kuu kama mwanamke ni kuwa na mtoto, kuona nakuwa chanzo cha maisha ya mtu na kutunza familia,” Rosa Ree aliiambia A-FM ya Dodoma.

Mkali huyo aliyasema hayo katika Siku ya Wanawake Duniani, ambapo alijumuika na wanawake wengine kuendeleza gurudumu la kutafuta usawa na ukombozi wa kiuchumi kwa wanawake wote wakisisitiza kuwa na umoja.

Rosa Ree alichaguliwa na kampuni moja ya kinywaji kuwa miongoni mwa wapa wanne Afrika ambao walishiriki katika kutengeneza wimbo mmoja kuhusu wanawake, uliopewa jina la ‘UNITY’ (umoja), ulioachiwa rasmi Machi 8.

“Mheshimu mwanamke usisahau ulipotoka, mwanamke amekupa maisha jichunge kabla ya kufoka,” ni sehemu ya ushairi wa Rosa Ree kwenye wimbo huo.

Lowassa anena awaomba waliompa kura mil.6 warudi CCM
Polepole ‘alivyomfagilia’ Lowassa

Comments

comments