Kikosi cha mabingwa wa soka barani Ulaya, klabu ya Real Madrid kimepata nguvu baada ya kureja mazoezini kwa washambuliaji Cristiano Ronaldo na Gareth Bale.

Wawili hao walikosa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Espanyol ambao walikubali kibano cha mabao mawili kwa sifuri, lakini kurejea kwao huenda kukaongeza chachu ya kusaka ushindi mwingine katika mchezo wa kesho dhidi ya Villarreal.

Ronaldo alikosa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita, kufuatia ugonjwa wa mafua uliokua unamkabili, ili hali kwa upande wa Bale alikua na tatizo la maumivu ya sehemu ya pembeni mwa paja (Hip).

Kwa sasa Real Madrid ambao wanaongoza msimamo wa ligi ya nchini Hispania, wamepania kuweka rekodi ya kushinda michezo 17 mfululizo ya ligi hiyo, baada ya kuifikia rekodi ya wapinzani wao FC Barcelona ya kushinda michezo 16 mfululizo.

FC Barcelona waliweka rekodi ya kucheza michezo 16 mfululizo bila kupoteza katika msimu wa 2010-2011.

Kikosi cha gwiji wa soka kutoka nchini Ufaransa Zinedine Zidane, kwa sasa kipo kileleni kwa tofauti ya point tatu dhidi ya FC Barcelona ambao kesho watawakaribisha Atletico Madrid huko Camp Nou.

Wenger: Nilishangaa Kuona Bendtner Amesaini Nottingham Forest
Dele Alli Anogewa Spurs, Ajifunga Hadi 2022