Mshambuliaji wa Manchester United Romelu Lukaku hatokua sehemu ya kikosi cha klabu hiyo katika mchezo dhidi ya Brighton and Hove Albion utakaochezwa kesho huko Falmer Stadium.

Lukaku mwenye umri wa miaka 24, alishindwa kumaliza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Arsenal, baada ya kutolewa kipindi cha pili kufuatia kuumia kifundo cha mguu, amethibitika hatoweza kucheza kesho.

Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amesema mshambuliaji huyo ambaye tayari ameshaifungua klabu yake mabao 16 na kutoa pasi za mwisho 34, huenda akawa fit kucheza tena, katika mchezo wa fainali wa kombe la chama cha soka nchini England (FA CUP), dhidi ya Chelsea baadae mwezi huu.

Jana Lukaku aliweka picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa katika kliniki ya Move to Cure nchini Ubelgiji, akiendelea kupatiwa matibabu ya jeraha lake.

“Hatokuwa sehemu ya kikosi kesho, anaendelea vizuri kupatiwa matibabu na ninaamini atarejea kwa wakati ili kumalizia msimu huu wa 2017/18,” Amesema Mourinho katika mkutano na wandhishi wa habari.

Katika mchezo dhidi ya Arsenal nafasi ya Lukaku ilichukuliwa na kiungo Marouane Fellaini ambaye alifanikiwa kuifungia Man Utd bao la pili na la ushindi dakika za lala salama.

Katika hatua nyingine beki kutoka nchini Ivory Coast Eric Bailly, ambaye  amekosa michezo mitatu ya ligi, huenda kesho akacheza dhidi ya  Brighton and Hove Albion.

Wizara ya Habari yafungua milango kwa wanahabari
Majaliwa anena kuhusu Dodoma kupewa hadhi ya jiji na JPM