Aliyekua kiungo wa timu ya taifa ya Argentina, Juan Roman Riquelme, amesema katika maisha yake ataendelea kujutia hatua ya kukataa kujiunga na klabu ya Man Utd mwaka 2006.

Riquelme, ambaye ameitumikia timu ya taifa ya Argentina katika michezo 51 na kufunga mabao 17, amesema aliikataa ofa ya Man Utd wakati akiwa nchini Hispania na klabu ya Villareal ambapo kwa wakati huo ilikua ikinolewa na meneja kutoka nchini Chile, Manuel Pellegrini.

Riquelme, amesema aliikataa ofay a klabu ya Man Utd wakati kikosi cha Villareal kilipokwenda jijini London kwa ajili ya kupambana na Arsenal katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingw abarani Ulaya.

Amesema wakiwa hotelini viongozi wa klabu ya Man utd walimfuata na kumumba akubalia kujiunga nao kwa msimu uliofuata wa 2006-07, lakini alionyesha msimamo wa kuwakatalia kwa akuamini alipokua akipafanyia kazi palimtosha.

Amesema maamuzi hayo yalitokana na mazingira maruzi ya kimaisha ambayo alikua akiyapata alipokua El Madriga ambapo aliishi vizuri na wachezaji wenzake.

Kukataa kwa kiungo huyo kulitoa nafasi kwa Man Utd, kumsajili kiungo kutoka nchini England, Michael Carrick, na walifanikiwa kumuhamisha akitokea Tottenham.

Mwaka mmoja baadae Riquelme aliondoka nchini Hispania na kurejea nyumbani kwao Argentina na kujiunga na klabu ya Boca Juniors ambapo alikua miongoni mwa wachezaji ambao waliiwezesha klabu hiyo kutwaa ubingwa wa Copa Libertadores.

De Gea Kuhudhuria Mazoezi Ya Man Utd Hii Leo
Steven Gerrard Akaribishwa Kwa Pombe Marekani