Kundi la wanaharakati wenye imani ya Kiislam nchini Ghana limeitaka Serikali ya nchi hiyo kumzuia Rihanna kukanyaga nchini humo kwa madai kuwa anahamasisha ushoga na waabudu shetani (freemasons).

Rihanna anatarajia kuhudhuria mkutano wa masuala ya elimu leo akiongozana na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron.

Mwimbaji huyo ni balozi wa kampeni ya kuchangia sekta ya elimu barani Afrika akihamasisha nchi za magharibi na watu wenye ukwasi kuchangia fedha kwenye sekta hiyo, kupitia mfuko maalum.

Hata hivyo, umoja wa taasisi 30 zinazojitanabaisha kuwa zinapinga ushoga na imani ya Freemasons umeitaka Serikali hiyo kumzuia kwani amekuwa akijiweka wazi kuwa ni muumini wa masuala hayo.

“Rihanna hafichi, ni sehemu ya Illuminate na tawi la Freemasons,” Cheikh Oumar Diagne, msemaji wa taasisi hizo amewaambia waandishi wa habari.

Mkutano huo ambao ni sehemu ya muugano wa kimataifa wa kuchangia elimu, umepanga kutafuta kiasi cha dola bilioni 2 ($2bn) kila mwaka, kusaidia nchi takribani 65 ndani na nje ya bara la Afrika kufikia mwaka 2020.

Tahmeed yapata ajali Tanga
Sirro atoa maagizo mazito