Mbunge wa Jimbo la Chalinze wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amewataka wazazi jimboni humo kuwahamasisha watoto wao kusoma masomo ya Sayansi ili kuweza kuisaidia serikali katika sehemu mbalimbali nchini.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha pili kutoka shule ya Sekondari Mboga iliyopo jimboni humo alipokwenda kuangalia maabara iliyojengwa kwa msaada wa mfuko wa jimbo na wananchi kwa lengo la kuinua wanasayansi jimbo la Chalinze

Amesema kuwa wazazi wana nafasi kubwa ya kuwashawishi watoto kutokana na wao kuwa nao muda mwingi majumbani na hata kutambua ndoto zao za mbeleni.

Aidha, ameongeza kuwa kuelekea Tanzania ya viwanda, ni lazima watahitajika wanasayansi wengi katika viwanda ili kuweza kuendeleza uzalishaji huo.

“Naipongeza serikali yangu ya awamu ya tano kwa kusisitiza ujenzi wa viwanda nchini kwa madhumuni ya kuongeza ajira kwa vijana wetu,”amesema Ridhiwani

Hata hivyo, kwa upande wake Afisa Elimu wa halmashauri ya Chalinze, Timoth Bernad amewataka wanafunzi wa shule hiyo kuitumia maabara kama ilivyo kusudiwa ili kuzalisha wanasayansi wa kutoka shule hiyo.

 

 

Video: Siasa za Maendeleo za CCM zamng'oa Mtatiro (CUF)
Bashir kugombea tena urais Sudan

Comments

comments