Rapa Rick Ross amewashtua mashabiki wa Diamond baada ya kufuta picha zote za mwimbaji huyo alizowahi kuweka kwenye akaunti yake ya Instagram.

Bosi huyo wa MMG, amezifuta kwa kuzichagua picha za Diamond pekee kwenye mtandao huo, ambazo aliwahi kuziweka tangu mwaka jana baada ya Bosi huyo wa WCB alipotangazwa kuwa ni balozi wa kinywaji cha ‘Balaire’ ambacho Ross anauhusiano nacho wa karibu.

Picha nyingine za Diamond ambazo Rick Ross ameziondoa ni zile zilizokuwa zinawaonesha wakiwa pamoja wakati wa kufanya video ya ‘Wakawaka’, wimbo ambao mkali huyo wa Ngololo alimshirikisha.

Kufuatia hatua hiyo, mashabiki wa Diamond wamemiminika mtandaoni kuhoji kilichojiri wasipate majibu ya haraka kuondoa kiu yao.

“Je ni uhasama? @richforever & @diamondplatnumz tuambieni tafadhali nini kimetokea kati yenu!! Kwani tulipenda muwe pamoja kwa ajili ya mafanikio zaidi. Mna wimbo pamoja #Waka. Leo dunia inashuhudia @richforever amefuta picha zote za @diamondplatnumz kwenye akaunti yake, hii ina maana gani?,” tafsiri isiyo rasmi ya ujumbe wa mdau wa muziki anayetumia jina la @dijacsonloyal.

Inaonekana Rick Ross amezichagua kwa makusudi picha za Diamond kwani ameacha picha za mabalozi wengine wa kinywaji hicho kama mrembo wa Kenya, Huddah Monroe.

Trump atuma salamu kwa viongozi Afrika
Mbowe: Dkt. Mollel alikuwa gunia la misumari Chadema