Meneja mpya wa klabu ya Arsenal Unai Emery anatazamia kuwasilisha ofa ya usajili wa beki wa pembeni kutoka nchini Uswiz na klabu ya AC Milan ya Italia Ricardo Rodriguez.

Mipango ya usajili wa beki huyo, imekuja kufuatia kuumia kwa beki wa pembeni wa Arsenal Sead Kolasinac, ambaye anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma kumi.

Beki huyo alipatwa na maumivu ya goti, wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Chelsea mjini Dublin, juma lililopita.

Hata hvyo inaelezwa kuwa, uongozi wa AC Milan huenda ukaweka ngumu kumuuza beki huyo mwenye umri wa miaka 25, na kama utakubali thamani yake haitoshuka zaidi ya Pauni milioni 30.

Rodriguez alielekea Italia mwanzoni mwa msimu uliopita, baada ya kucheza katika ligi ya Ujerumani kwa muda wa miaka mitano akiwa na klabu ya Wolfsburg.

Sababu nyingine ya usajili wa beki Rodriguez kupewa nafasi ya kusajiliwa huko Emirates Stadium, ni kutokana na beki wa kushoto wa kutumainiwa katika kikosi cha Arsenal Nacho Monreal, kutokua sehemu ya kikosi katika kipindi hiki kufuatia majeraha ya goti aliyoyapata akiwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania kilichosriki fainali za kombe la dunia.

Juma hili beki huyo anatarajiwa kurejea London kuanz amazoezi mepesi, na huenda ikamchukua majuma kadhaa kuwa FIT, kwa ajili ya kuanza kupambana katika mshike mshike wa ligi kuu nchini England ambao utaanza Ijumaa.

Kwa mantiki hiyo beki huyo hatoweza kuwa sehemu ya kikosi cha The Gunners kitakachoanza ligi kuu msimu wa 2018/19 mwishoni mwa juma hili kwa kuwakabili mabingwa watetezi Man city.

Beki kinda Ainsley Maitland-Niles anapewa nafasi kubwa ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.

Mwongozo rahisi wa kutatua migogoro kazini
Niko Kovac ampinga bosi wake FC Bayern Munich