Rais Dkt. John Magufuli amesema Serikali yake imeamua kuboresha miundombinu nchini ikiwepo ujenzi wa reli ya kisasa kwaajili ya treni ya umeme ambayo amepanga katika awamu ijayo mradi huo utafika Mwanza na Arusha.

Amebainisha hayo leo, Juni 29 Kilosa mkoani Morogoro, wakati akihutubia wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mahandaki kwaajili ya reli hiyo, kipande cha kutoka Morogoro hadi Makutupora Dodoma.

” Katika kipindi kinachokuja kingine, tutaanza ujenzi wa reli kutoka Mwanza hadi Makutupora, nayo tutaigawanya katika sehemu mbili, reli ya kwenda Arusha, sasahivi treni inafika huko ili watu tuwape uwezo wa kuchagua, tutaendelea pia kushughulikia na maeneo mengine” Amesema Magufuli.

Amesema sababu kuu ya kuamua kuborasha miundombinu ni kwakuwa anatambua ndiyo roho ya taifa katika maendeleo hivyo wananchi wanatakiwa kuisimamia na kulinda amani ya nchi bila kubagua, dini, wala chama kufanikisha maendeleo.

Aliyetaka mkewe amrudishie figo aliyompa baada ya kudai talaka ‘akwaa kisiki’
Magaidi wauawa katika shambulizi Pakistan