Siku moja kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la dunia nchini Urusi, shirikisho la soka nchini Hispania limetangaza kumfuta kazi kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo Julen Lopetegui.

Maamuzi ya kufutwa kwazi kwa Lopetegui, pia yamekuja baada ya kutangazwa kuwa mkuu wa benchi la ufundi la mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Hispania zinaeleza kuwa, Lopetegui amefutwa kazi ili kuepuka kuleta mkanganyiko ndani ya kikosi cha timu ya taifa hilo, ambacho tayari kimeshawasili nchini Urusi kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia.

Lopetegui alihofiwa huenda angeshindwa kuwapa nafasi wachezaji wa FC. Barcelona na Atletico de Madrid ambao wapo kikosini kwa sababu ya upinzani baina ya klabu hizo na Real Madrid.

Rais wa Shirikisho hilo, Luis Rubiels mapema leo aliitisha kikao na viongozi wenzake ili kujua mustakabali wa Lopetegui baada ya kutangazwa na Real Madrid kuchukua mikoba ya Zinedine Zidane.

Bodi ya Shirikisho hilo pamoja na Rais wameazimia kumfuta kazi kocha huyo na badala yake atatangazwa kocha mwingine kurithi nafasi yake ili kukiongoza kikosi kwenye michuano hiyo mikubwa duniani.

Marekani, Canada na Mexico wenyeji kombe la dunia 2026
Makala: Jitambue, tambulika, fahamu undani wa ubunifu wa mavazi