Vigogo wa soka nchini Hispania Real Madrid na FC Barcelona, usiku wa kuamkia leo waliangusha vipigo vya mbwa mwizi katika michezo ya La Liga.

Real Madrid walikua ugenini wakicheza dhidi ya Derpotivo la Coruna na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 6-2, huku FC Barcelona wakiwakandamiza Osasuna mabao 7-1 kwenye uwanja wa Camp Nou.

Mabao ya Real Madrid yalikwamishwa wavuni na James Rodrigues aliefunga mabao mawili huku Alvaro Morata, Lucas Vazquez, Isco na Casemiro kila mmoja akitupia.

Derpotivo nayo ilijitutumua na kupata mabao mawili kupitia Florin Andone na Joselu ingawa hayakusaidia kubadili matokeo ya kuokata pointi tatu nyumbani.

Upande wa FC Barcelona, Lionel Messi alinyesha hakubahatisha katika mchezo wa El Clasico dhidi ya Real Madrid, baada ya kufunga mabao mawili miongoni mwa mabao saba yaliyowapa ushindi dhidi ya Osasuna.

Wakati Messi akipiga mabao mawili, Andre Gomes naye alitupia mbili na Francisco Alcacer naye akatupia mbili na kukamilisha hesabu ya mabao sita.

Lakini beki kisiki raia wa Argentina, Javier Mascherano, naye akapiga moja kukamilisha hiyo hesabu ya wiki.

Korea Kaskazini 'yashindilia msumari' baada ya Marekani kupeleka Meli za Kivita
FC Bayern Munich Watupwa Nje DFB Pokal