Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mawnri ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Maofisa Ustawi wa Jamii wa  Wilaya zote kuhakikisha wamekamilisha zoezi la kuwatambua na kuwapatia vitambulisho vya matibabu kwa wazee wote ambao wana umri wa  miaka 60 kuendelea.

Ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wazee Mkoani humo na baada ya takwimu za waliopatiwa vitambulisho hadi sasa kuwa kidogo wakati wazee wengi wakiwa bado hawajapatiwa.

Amesema kuwa kati ya wazee 74,454 waliotambuliwa  ni 26,000 ndio wameshapata vitambulisho hivyo na kuongeza kuwa wengine bado hawajatambuliwa.

Aidha, Mwanri amesema kuwa katika zoezi hilo la kuwatambua na kuwapatia vitambalisho hakuna kumuacha mzee hata mmoja aliye na sifa kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Wazee ya Mwaka 2003.

Hata hivyo, ameongeza kuwa baada ya mwezi mmoja kupita Afisa Ustawi wa Jamii ambaye atakutwa katika Halmashauri yake kuna wazee wenye sifa hawana vitambulisho ajue hana kazi.

Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tabora Msalika Makungu alisema Serikali inawategemea sana wazee hao katika kutoa ushauri ili watendaji wafanye maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Idriss aunga mkono muziki wa Hamisa Mobetto, wengine wamponda
DC Mjema aunda mkakati wa kudhibiti uhalifu Ilala