Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme amesitisha likizo zote wa watendaji wakuu wa mkoa na wilaya ili wasimamie ujenzi wa madarasa mapya kwenye shule za sekondari ili kuwezesha mkoa wake uwezeshe wanafunzi wote watakaofaulu mwaka 2019 kuendelea na masomo.

Mndeme ametoa agizo hilo wakati wa kikao chake na viongozi na watendaji wa taasisi za umma na binafsi kwenye ukumbi wa Manispaa ya Songea na kuwataja viongozi ambao hawapaswi kwenda likizo hadi vyumba vipya 142 vikamilike kujengwa.

Aidha, viongozi waliozuiwa kwenda likizo ni Katibu Tawala Mkoa, Wakuu wote wa wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, Afisa Elimu Mkoa na wale wa wilaya zote pia wahandisi wa ujenzi wa halmashauri.

“Nataka katika halmashauri zote zenye upungufu wa vyumba madarasa hakuna kiongozi kwenda likizo ya mwisho wa mwaka hadi madarasa mapya yakamilike kujengwa ili wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2019 waingie darasani ,”amesema Mndeme

Awali akitoa taarifa fupi ya hali ya miundombinu ya madarasa Katibu Tawala Mkoa, Prof. Riziki Shemdoe amesema kuwa jumla ya wanafunzi wapya 1,556 watahitaji madarasa mapya ya kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari.

Hata hivyo, Prof. Shemdoe amezitaja halmashauri zenye upungufu wa madarasa na idadi kwenye mabano kuwa Tunduru(35), Mbinga (18), Songea (09), Songea Manispaa (09),Namtumbo (26), zingine ni pamoja na Halmashauri ya Nyasa (32), Mbinga Mji (09) na Madaba (04)

Chadema yamjibu Makonda, 'hawakupewa mialiko'
Real Madrid kuukimbia mzimu wa Eibar leo?