Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda rasmi amezindua mfumo wa kuratibu malalamiko ya wananchi wake wa mkoa wa Dar es salaam ambayo yatakuwa yakiwasilishwa kwa kutumia simu ya mkononi na kompyuta.

Amesema kuwa kupitia simu hiyo ya mkononi malalamiko au kero hizo zitakuwa zinatumwa kwenda nambari 11000 kwa kuanza na neno DSM, na kwa kutumia kompyuta unaweza kutuma malalamiko hayo kupitia tovuti yao ya www.malalamiko.dsm.co.tz.

Ambapo kuanzia sasa wana Dar es salaam wanaweza kufikisha kero zao, malalamiko yao moja kwa moja ofisini kwa mkuu wa mkoa na kufanyiwa kazi.

”Mkoa sasa umeamua kuhamia nyumbani kwako, ni simu yako tu ya mkononi, unaweza kutuma malalamiko yako, kero zako kwa kuanza na neno dsm au kifupi cha Dar es salaam ukishaandika dsm unaenda kutuma kwenda namba 11000, ndio namba ambayo tutaitumia kupokea malalamiko, kero au umeenda kwenye ofisi ya uma hujapata huduma nzuri au upo nyumbani kuna jambo limekutatiza unaona ni vyema kutoa taarifa katika uongozi wako wa mkoa” amesema Makonda.

Ameenda mbali zaidi kwa kusema kwamba hata kama umeenda ofisi za umma na kupata huduma mbovu ni vizuri kuwasilisha malalamiko hayo ili yaweze kufanyiwa kazi.

Aidha, kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wananchi hivyo uzinduzi wa utaratibu huo utasaidia kufikisha kero za wananchi kwa wakati sahihi na kufanyiwa kazi pia.

Hata hivyo kumekuwa na malalamiko mengi sana kutoka kwa wanachi juu ya watoa huduma katika ofisi za serikali kukosa ushirikiano kwa watu wanaotembelea ofisi hizo kwa kupata huduma, nadhani kupitia utaratibu huu aliouanzisha mkuu wa mkoa itakuwa ni mwarobaini wa wafanyakazi wa umaa ambao hawana huduma nzuri kwa watu wanaotembelea ofisi hizo.

 

 

Wananchi watishia kugomea uchaguzi wa serikali za mitaa
Takukuru yampandisha kizimbani mhadhiri aliyefumaniwa mtupu gesti akiomba rushwa ya ngono