Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameanza maandalizi kuelekea mkutano mkuu wa nchi za SADC, unaotarajia kufanyika Agosti 2019 jijini Dar es salaam, ambapo amekutana na waendeshaji wa mitandao ya kijamii na kuwakabidhi maswali 12, kwa ajili ya kuwauliza wananchi kuelekea mkutano huo.
 
Makonda amefikia maamuzi hayo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa lengo la mkakati huo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na uelewa kuhusiana na mkutano wa SADC, pamoja na kujua kiundani juu ya umuhimu wa mkutano huo kwenye masuala ya biashara.
 
“Tufanye jambo litakalotikisa Mkoa wetu, nataka tufanye mashindano yatakayokuwa na zawadi, zawadi ya kwanza itakuwa wewe na kamera yako, na zawadi ya pili itaenda kwa mwananchi utakayefanya naye kazi.”amesema Makonda
 
Aidha, amesema kuwa zawadi ya mshindi ataitoa tarehe 5, Agosti mwaka huu, hivyo amesisitiza kwa mwenye uwezo wamsaidi kupatikana kwa majibu hayo ya maswali 12 na mwisho wa siku atajichukulia milioni 3.
 
Hata hivyo, Makonda amewatoa hofu wamiliki wa mitandao hiyo ya kijamii kwamba wanaweza kukamatwa wakati wa kutekeleza majukumu yao.
Kamanda Mambosasa aelezea ‘mashaka’ kutekwa kwa msaidizi wa Membe
Wimbo wa Beyonce wenye Kiswahili waiinua filamu ya 'The Lion King', usikilize hapa

Comments

comments