Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Salum Hapi amekutana na wazee wa mkoa huo na kusimikwa rasmi kuwa Chifu wa Wahehe kama ishara ya kumpokea na kumpa nguvu ya kutawala mkoa huo.

Katika mkutano huo uliofanyika ukumbi wa siasa na Kilimo uliopo mkoani humo, wazee wa mkoa huo wamejitokeza kwa wingi ili kuweza kumsimika mkuu huyo wa mkoa.

“Mhe Rais amenituma niwape salamu zake. Lakini pia amenipa kazi ya kuhakikisha tunawatumikia na kutatua kero zenu ili wana Iringa mjivunie kuwa hamkukosea kumchagua Rais Magufuli na mjisikie fahari na nchi yenu. Siku zote nitasimama upande wenu wananchi na hasa wanyonge,”amesema Hapi

Aidha, Hapi ametoa fursa kwa wazee hao kueleza matarajio yao na changamoto zao ambazo wangependa serikali ya mkoa izifanyie kazi.

Hata hivyo, Wazee wamemueleza RC Hapi changamoto za huduma zisizoridhisha hospitali ya Mkoa, majibu mabaya ya watoa huduma, migogoro ya ardhi, Maji na mikopo ya kina mama na ucheleweshwaji wa pembejeo kwa wakulima.

 

Kwasasa mimi ni balozi wa Rais Dkt. Magufuli- Mtatiro
Hasunga awatuliza wananchi kuhusu mipaka ya pori la Selous

Comments

comments