Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amesema kuwa ataendelea na msimamo wake katika kuhakikisha anasimamia sheria ili shughuli za maendeleo ziweze kufanyika katika jiji la Mbeya.

Ameyasema hayo jijini humo wakati wa ziara ya Rais Magufuli inayofanyika mkoani Mbeya, ambapo amesema kuwa amekuwa akiingia majaribuni mara kwa mara hususani kupitia watu wenye vipato vikubwa kwa nia ya kumuhonga lakini amekuwa akiwaagiza wapeleke fedha hizo kwenye miradi ya maendeleo.

”Tukisiamamia sheria tutalifikisha taifa hili mbele, inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wanaleta unafiki katika kusimamia sheria hii sio nzuri hata kidogo, tangu Rais Magufuli aliponiteua sijawahi kukaribisha kiumbe chochote kije kinipe utajiri mfukoni mwangu, watu walionyesha nia, nikawaambia wapeleke kwenye mashule lakini mshahara unaonipa napata mshahara wa kukaa na hata mchepuko kidogo,”amesema Chalamila.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya mara kwa mara amekuwa akiingia kwenye mvutano wa maneno na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) ambapo mara nyingi imekuwa ikisababishwa na mivutano ya kisiasa.

Video: Wakili Manyama amshukia Zitto Kabwe, 'Hatakiwi kupotosha umma'
Video: Chege atoboa siri kumfukuzia Vanessa miaka mitatu

Comments

comments