Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila ameamua kuingilia kati Bodi ya Shule ya Sekondari Kiwanja na kuwasimamisha shule wanafunzi wa kidato cha 5 na 6 kwa muda wa wiki mbili kwa kisa alichotaja kuwa wanafunzi hao wanaongoza kwa kumiliki simu shuleni kinyume na sheria.

Katika shule hiyo kidato cha 5 na 6 kuna jumla ya wanafunzi 392 ambapo mbali na adhabu hiyo pia amewataka wanafunzi hao pindi watakaporejea shule waje na kiasi cha pesa cha shilingi 200,000 kwa kila mwanafunzi huku wale wanafunzi walioshikwa na simu kuja na shilingi 500,000 pamoja na wazazi wao ambapo kiasi hiko cha pesa wameelekezwa kuweka katika akaunti ya shule.

”Kwahiyo kutoka sasa nafunga Form 5 na 6 mnaondoka kwenda kwenu naikifika saa 4 saa 5 watu wanang’aang’aa hapa mtakung’utwa kichapo cha kufa mtu, Bodi ilipaswa iwe imekwisha kaa tangu siku ya kwanza ilipotokea tukio, sasa naiamulia bodi nawaamuru na nyinyi wanafunzi wote mtakuja na laki mbilimbili na wote waliokuwa na simu hizi mtakuja na laki tano tano na wazazi juu” amesema RC Chalamila.

Mkuu wa mkoa alItembelea shule hiyo na kupokea ripoti hiyo kutoka kwa mkuu wa shule ambapo aliamua kuwacharaza viboko wanafunzi 14 waliokutwa na simu huku wanafunzi wengine 5 kushikiliwa na jeshi la polisi kwa taarifa zaidi.

Aidha kumekuwa na minong’ono mingi kuhusu kitendo hiko kilichofanywa na mkuu wa mkoa hivyo mapema leo ametoa ufafanuzi na kusema kuwa ni kweli Mkuu wa shule ndiye anatakaiwa kumchapa mwanafunzi lakini Mkuu wa Mkoa ni bosi wa mkuu wa shule hivyo Mkuu wa Mkoa alitakiwa awachape zaidi wanafunzi hao.

Pia ameomba askari kuendelea kutoa ulinzi mkali kwa shule hiyo mara baada ya kuwasimamisha shule vijana 392 wa kidato cha 5 na 6 kwa utomvu wa nidhamu ili kuendelea kuweka usalama wa shule.

”Shule hii afande ilindwe ili kijana yeyote atakayefanya jaribio lolote ni kutandikwa kweli kweli kwa mujibu wa sheria na kanuni zenu” amemalizia Chalamila.

Jibu la chadema kwa msajili wa vyama lawekwa bayana
Isaac Promise afariki dunia, Ferdinand amlilia