Msanii wa muziki kutoka kundi la WCB, Rayvany amefungiwa wimbo wake wa Mwanza kwa mara ya kwanza na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) aliomshirikisha msanii mwenzake Diamond platnumz ambao unakiuka maadili ya Kitanzania.

Siku ya jana Baraza La Sanaa Tanzania lilitangaza rasmi kufungia wimbo huo unaokiuka maadili ya kitanzania kulingana na maneno yaliyotumika kwenye wimbo huo.

Aidha, baada ya kufungiwa wimbo huo, Rayvany ameibuka na kulalamikia uamuzi huo wa Basata na kusisitiza kuwa haikuwa maana yao kuimba matusi bali ni sanaa iliyotumika.

“Dhamira yetu haikuwa kama inavyoonekana sasa, dhamira yetu ilikuwa ni kutoa burudani kwa hadhira iliyokusudiwa  amabo ni vijana wenzetu”ameandika kwenye ukurasa wake wa Instagram

Hata hivyo, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) hapo jana liliufungia wimbo huo ambao unakiuka maadili ya Kitanzania na kumtaka msanii huyo kuutoa wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii.

Muungano wa vyama vya upinzani Congo DR wasambaratika
Rostam Azizi atinga Ikulu kuonana na JPM