Shirikisho la mpira Duniani FIFA limebadili utaratibu wa namna ya kupanga makundi katika fainali za Kombe la dunia 2018 nchini Urusi.

FIFA imesema wakati wa kupanga makundi itazingatia viwango vya soka ambavyo huwa inavitoa kila mwezi kwa timu za taifa ambapo sahani (Pot) zote 4 zitapangwa kulingana na viwango kwenye orodha ya FIFA. Awali sahani ya kwanza pekee ndio ilikuwa inazingatia viwango hivyo lakini sasa itakuwa ni kwa sahani zote.

Pia FIFA imethibitisha kuwa itatumia viwango itakavyotoa mwezi Oktoba. Hii inamaanisha sahani ya kwanza huenda ikawa na timu za Ujerumani, Brazil, Ubeligji, Argentina, Ureno pamoja na wenyeji Urusi, lakini hadi sasa Brazil na Ubeligji pekee kwenye nchi za juu ndio zimefuzu.

Kuna dalili kubwa ya mataifa ya Uingereza, Hispania na Ufaransa yakawa katika sahani ya pili endapo yatafuzu. Afrika Mashariki katika kuwania kufuzu inawakilishwa na Uganda pekee ambayo ipo nafasi ya pili kwenye kundi E ikiwa na alama 7 nyuma ya Misri yenye alama 9. Uganda inashika nafasi ya 71 kwenye viwango vilivyotolewa jana na FIFA wakati Tanzania ikiwa nafasi ya 125.

Gwajima afutiwa keshi iliyokuwa ikimkabili
Video: Nas na Nick Minaji katika mahusianao?

Comments

comments