Mtayarishaji wa Muziki nchini Rash Don afunguka kuwa Studio ya Suprise Music ni Studio yake pamoja na msanii Rayvanny kutoka kundi la WCB.

Rash Don amesema kuwa mipango ya kufungua Studio ilikua niya muda mrefu na alipo maliza mkataba wake na Studio ya Kiri Records ndipo akaamua kuungana na Rayvanny kufungua studio waliyoipa jina la Surprise Music.

”Studio ya Surprise ni studio ambayo tumeifungua kwa kushirikiana na Rayvanny kwakuwa ni msanii ambaye nimekuwa nae tangu tulipokuwa Mbeya ambako ndio tulifahamiana na hili wazo la kufungua studio tulikuwa tumelipanga tangu awali” amesema Rash Don.

Hata hivyo Rash Don amefafanua juu ya jina la Surprise na kusema kuwa wameamua kutumia kwa sababu wanataka wafanye mambo makubwa na mazuri ambayo yatakuwa yanawashangaza mashabiki wa muziki kutoka Surprise Music.

Rash don amesha fanya kazi na wasanii wengi na wakubwa katika muziki huu wa kizazi kipya  na miongoni mwa wasanii ambao tayari amesha fanya nao kazi ni pamoja na Stamina, Chid Benz, Country Boy, Stereo na wengine wengi.

Mpaka sasa studio ya Surprise Music imekwisha toa wimbo mmoja wa msanii Dogo Janja unao itwa Ngarenaro wimbo ambao unafanya vizuri kwa sasa huku ukiwa umetayarishwa na Rash Don.

Video: Jeshi la polisi kula sahani moja na wahalifu wa mitandaoni
Conte aitabiria Arsenal ubingwa

Comments

comments