Mkongwe wa muziki wa HipHop nchini Marekani 50 Cent amegonga vichwa vya habari, hii ni baada ya kumkana hadharani kijana aitwaye Marquise Jackson (21) anayedaiwa kuwa ni mtoto wake.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram 50 Cent amesema kuwa kijana huyo sio mtoto wake na tayari ameshapima damu kuhakikisha hilo.

“Yule sio mtoto wangu, Nimeshapima damu. Nitolee upumbavu wako hapa,“ameeleza 50 Cent kwa kumjibu shabiki yake ambaye aliuliza kwanini? 50 Cent kwenye show yake na Snoop Doggy walimbania mtoto wake Marquis Jackson asiingie backstage na kumuacha nje kwenye viti vya kawaida.

Marquise Jackson mwaka jana aliposti picha akiwa na mtoto wa Supreme McGriff ambae ni hasimu wa muda mrefu wa rapa 50 Cent jambo ambalo lilimkwaza rapa huyo wa HipHop na akashindwa kuzuia hisia zake na kukomenti kwenye post hiyo kwa kuandika, “Hata kama watu hawa wawili wakigongwa na gari, Kwangu haitakuwa siku mbaya,“.

Mchungaji ajivua uchungaji kwa kesi ya ubakaji
Rais Magufuli aenda Chato kwa mapumziko

Comments

comments