Rais wa Sudan, Omar al-Bashir ameendelea kuikosesha usingizi Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) inayotaka akamatwe kwa makosa ya jinai dhidi yake, baada ya kuhudhuria kikao cha ‘Eneno Huru la Biashara la Ukanda wa Afrika (AfCFTA) jijini Kigali nchini Rwanda.

Sudan iliungana na nchi nyingine 43 za Afrika kusaini makubaliano ya AfCFTA yenye lengo la kuufanya ukanda wa Afrika kuwa eneo huru la biashara kwa kuondoa vizingiti vya kibiashara kati ya nchi hizo.

Mpango huo ambao ni sehemu ya ajenda ya mradi wa kufanikisha ifikapo mwaka 2063 utahuisha ushirikiano wa kibiashara kati ya nchi hizo kwa kuwawezesha waafrika kufanya biashara bila kulipa tozo kadhaa.

ICC inamtafuta Bashir tangu mwaka 2008 kwa tuhuma za mauaji ya kimbali na makosa dhidi ya haki za binadamu. Anatuhumiwa kutenda makosa hayo jijini Darfur.

Mahakama hiyo imekuwa ikizisihi nchi anazotembelea kumkamata lakini haijafanikiwa. Bashir amekuwa akitembelea nchi kadhaa barani Afrika ikiwa ni pamoja na Uganda, Misri na Rwanda.

Waziri asimamishwa kazi kwa muda
Nchi 44 Afrika zasaini makubaliano ya biashara huru