Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akiongozana na Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Rashid Ali Juma wamempokea Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infatino ambaye ameongozana na Rais wa CAF, Ahmad Ahmad.

Rais FIFA na ujumbe wake wamewasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa 10:20 alfajiri. ambapo Dkt. Mwakyembe amemhakikishia Rais huyo wa FIFA utayari wa Tanzania katika kushirikiana na kutekeleza miradi na mipango mbalimbali.

Kwa upande wake, Rais wa FIFA amemshukuru Waziri Mwakyembe kwa mapokezi mazuri aliyopata na kumhakikishia kuboresha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya Mpira wa Miguu.

Aidha, Rais wa FIFA alisema chaguo la kufanyia mkutano huo Tanzania limetokana na maendeleo ya kasi ya tasnia ya mpira wa miguu na weledi wa viongozi wa TFF waliopo madarakani.

Serikali yatoa msimamo juu ya milioni 80 mazishi ya Akwilina
Raia wazidi kutaabika nchini Burundi