Imeelezwa kuwa rais wa Botswana, Mokgweetsi Eric Masisi atakuwa Karantini kwa siku 14 baada ya kurudi nchini humo akitokea Namibia ambapo watu watatu wamethibitishwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Rais Masisi alienda Namibia kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais wa nchi hiyo, Hage Geingob. Viongozi wengine waliokuwepo ni pamoja na rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe na rais Joao Lourenco wa Angola.

Corona : Angela Merkel Karantini

Taarifa ya Serikali imesema rais Masisi atapimwa ili kufahamu kama ameambukizwa Covid 19, na atakuwa mbali na familia yake muda wote wa Karantini. Waliokuwa na rais huyo pia wametengwa na watapimwa

Akiwa nchini Namibia, Rais huyo pia alifanya kikao cha dharura na viongozi wa mataifa mengine kujadili hatua zinazochukuliwa ili kupambana na mlipuko wa Corona.

Kifo cha Dkt. Makongoro Mahanga, Chadema watoa taarifa

CORONA: Marouane Fellaini awekwa KARANTINI
Kifo cha Dkt. Makongoro Mahanga, Chadema watoa taarifa