Rais wa Urusi, Vladmir Putin amesema kuwa Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un yuko tayari kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu mpango wa nchi hiyo wa silaha za nyuklia.

Ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye hotuba ya televisheni baada ya kukutana kwa mazungumzo ya ana kwa ana na kiongozi huyo wa Korea Kaskazini mjini Vladivostok, ambapo Putin amesema kuwa atayajadili matokeo ya mkutano huo wa kilele na uongozi wa Marekani.

Amesema kuwa Urusi na Marekani zina maslahi ya pamoja katika kuitaka Korea Kaskazini iachane na silaha za nyuklia, akiongeza kuwa Kim amemuomba auwasilishe kwa mara nyingine tena kwa Marekani msimamo wa Korea Kaskazini kuhusu suala hilo.

Aidha, ziara ya Kim mjini Vladivostok inakuja wakati Korea Kaskazini ikiwatafuta washirika baada ya mkutano wa kilele kati ya Rais wa Marekani Donald Trump na Kim mjini Hanoi, Vietnam mwezi Februari ambapo viongozi hao wawili walishindwa kukubaliana kuhusu masuala muhimu kuhusiana na mpango wa kuondoa silaha za nyuklia.

Viongozi wakuu wa Baraza la Mpito la Kijeshi wajiuzulu Sudan
Video: Hoja ya Msukuma kwa Bongo Movie ni shuti, ya Zamaradi na Steve Nyerere..! (Makala)

Comments

comments