Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameshangazwa na lawama zinaendelea kuelekezwa kwa rais wa FIFA Sepp Blatter, kufuatia sakata la mlungula linalowahusu baadhi ya maafisa wa shirikisho hilo la soka duniani kote.

Putin, ambaye nchi yake itakuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2018, amesema haoni sababu za wadau wa soka duniani kuendelea kumuangushia lawama mzee huyo kutoka nchini Uswiz, kutokana na mambo mazuri ambayo ameifanyia duniani katika mchezo wa soka.

Putin, amesema Blatter ni msafi kati ya watu wasafi duniani na anastahili kutunukiwa tuzo ya Nobel, hivyo amewataka wadau wanaompinga kuacha mpango huo, na kufikiria ni vipi anavyousaidia mchezo wa soka duniani.

Sababu kubwa ya kiongozi huyo wa ngazi ya juu nchini Urusi, kujitokeza hadharani na kujaribu kumsafisha Blatter, imetajwa kuwa ni kuchoshwa na taarifa ambazo zimekua zikiendelea kuzungumzwa katika baadhi ya vyombo vya habari duniani, pamoja na kwa mtu mmoja mmoja kumuhusu kuongozi huyo wa FIFA.

Putin, amesisitiza kwamba, haiwezekani makossa ya watu wengine ndani ya FIFA yakawa mzigo kwa kiongozi wa shirikisho hilo ambapo mpaka sasa haijathibitika kama kweli alihusika na uchafu uliokua unafanywa na wasaidizi wake.

Kama itakumbukwa vyema shirika la upelelezi la nchini Marekani FBI, liliwakamata baadhi ya maafisa wa FIFA miezi miwiwli iliyopita huko nchini Uswiz baada ya kujiridhishwa na ushahidi wa kuwepo kwa rushwa ndani ya shirikisho hilo.

Blatter, amekua sehemu ya upelelezi unaendelea kufanywa na FBI na kama itabainika alihusika katika utaratibu za kujihusisha na masuala la rushwa kupitia shirikisho hilo atatiwa nguvuni.

Dkt Slaa Aelezea Mkutano Wa Chadema Na Lowassa, “Lowassa Sio Mgombea Wa Chadema”
Dkt. Salim Awaasa Wanasiasa Wanaochungulia Ikulu