Rais wa Malawi, Peter Mutharika amewataka wafuasi wake kupuuza ripoti zinazosema ameshindwa katika Uchaguzi wa marudio na kuwataka kusubiri matokeo rasmi ya Tume ya Uchaguzi ambayo bado hayajatangazwa.

Matokeo ya Wilaya zote yaliotiwa saini na Maafisa pamoja na wawakilishi yanaonesha Rais Mutharika yuko nyuma ya Lazarus Chakwera ambaye anaongoza Chama cha Upinzani cha Malawi Congress party, kinachowakilisha muungano wa vyama 8 vya upinzani.

Matokeo rasmi ya uchaguzi hayajatangazwa lakini chombo cha habari cha Serikali (MBC) kimesema kiongozi wa upinzani alikuwa anaongoza kwa 59% ya kura zilizohesabiwa Juni 24.

Ikumbukwe kuwa, Mwaka uliopita, Malawi ilikuwa nchi ya pili Barani Afrika kutengua matokeo ya Uchaguzi wa Urais kufuatia madai ya udanganyifu, baada ya Kenya 2017.

IMF kuipatia Tanzania fedha kukabili athari za Corona
Tanzania kuisaidia Burundi kujiunga SADC