Licha ya kushika nafasi ya tatu katika shindano la Miss World lililofanyika Sanya nchini China Disemba mwaka huu na kutwaa taji la Miss Afrika, mrembo wa Uganda Quiin Abenakyo amekula za uso toka kwa Rais Yoweri Museveni baada ya kukaribishwa Ikulu.

Quiin alipata mapokezi mazuri kutoka kwa Waziri wa utalii pamoja na Rais Museveni ambaye alikaribisha Ikulu kwa ajili ya kumpongeza kwa hatua alioyofikia kuitangaza vizuri Uganda na Afrika kwa ujumla katika mashindano hayo dunia.

Aidha Rais Museveni hakuishia tu kumpongeza mrembo huyo pia alimpa dongo kupitia ukurasa wake wa twitter katika picha ya pamoja na mrembo huyo mwenye urefu wa twiga.

“Abenakyo ni mrefu kweli kweli, msichana mzuri toka Musoga. Tatizo langu ni moja kwake, alikuwa amevaa nywele za Kihindi. Nimemsisitiza kwenye kubaki na Uasilia wake, nywele za Kiafrika. Lazima tuuoneshe uzuri wa Kiafrika kwenye muundo wake asilia.”ameandika katika ukurasa wake wa kijamii.

 

Video: Diamond, Rayvanny wapiga magoti, 'Ni kweli tumekosea'
Mbowe, Matiko wakwama, sasa kula Chrismas na mwaka mpya Gerezani

Comments

comments