Rais wa zamani wa Marekani, George H W Bush amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 94, mwanawe rais wa zamani pia George W Bush ametangaza hayo.

George Bush Senior, kama alivyofahamika sana, amefariki dunia mida ya saa nne na dakika kumi usiku (saa kumi na dakika kumi GMT)

Alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1993 baada ya kuongoza kwa mihula miwili kama makamu wa rais chini ya Rais Ronald Reagan.

Aidha, Aprili mwaka huu alilazwa hospitalini akiwa na matatizo ya ubongo na kwenye damu lakini akatibiwa na kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

George Herbert Walker Bush amefariki miezi saba tu baada ya kifo cha mke wake Barbara.

Viongozi mbalimbali wametuma salamu za rambirambi na kumkumbuka mwanasiasa huyo, wakiongozwa na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump aliyemsifu kwa uhalisia wake, ucheshi na kujitolea kwake kudumisha imani, kwa familia na kwa taifa.

Bendera katika ikulu ya White House zitapepea nusu mlingoti huku mipango ya mazishi ikiendelea.

Hata hivyo, alilaumiwa kwa kupuuza maswala ya ndani ya Marekani na kwa kupuuzilia mbali ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni ambapo aliahidi kuwa hataongeza kodi.

 

Wababe Deontay Wilder, Tyson Fury kuitikisa dunia leo
Video: Chanzo Mbowe na Matiko kurudi tena mahabusu, Burundi 'yavunja' kikao marais EAC

Comments

comments