Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi, Mawaziri wake pamoja na Wabunge wote wa Bunge la Nchi hiyo, wamewekwa karantini kwa siku 14 baada ya muuguzi aliyewapima dalili za corona viongozi hao kugundulika ameambukizwa.

Muuguzi huyo aliwapima kabla ya mkutano wao wa jumatano wa kujadili hali ya dhalula, imeelezwa kuwa alianza kuugua ghafla na matokeo ya vipimo yameonesha kuwa ana virusi vya corona.

Mkurugenzi wa wizara ya afya, Malaki Tshipayagae ndiye aliyetangaza agizo la kuwaweka viongozi hao karantini kwa siku 14 kupitia runinga ya taifa.

” Mnatakiwa kujiweka karantini nyumbani kwenu kama mtaweza, na mkishindwa tutawatafutia sehemu, tutawafanyia vipimo baada ya siku 14 mkiwa salama mtaruhusiwa kutoka” amesisitiza Tshipayagae

Botswana imethibitisha visa vya wagonjwa wa covid 19 hadi sasa 13, huku rais wao akitangaza hali ya dhalula kwa miezi sita.

Video: Wananchi wote kuvaa barakoa, Ni pasaka ya aina yake
Video: Takukuru yamulika maandalizi uchaguzi mkuu 2020