Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 30 kukamilika kwa ujenzi wa kituo cha mabasi Njombe kilichotumia zaidi ya miaka mitano na bado hakijakamilika.

Rais Magufuli amesema hayo leo Aprili 10, 2019 wakati kizungumza na wananchi katika ziara yake ambapo amemuagiza Mkuu wa Mkoa Njombe, Christopher Ole Sendeka kuhakikisha hadi ifikiapo Mei 10, 2019 kuhakikisha mradi huo wa stendi unakabidhiwa ukiwa umekamilika kwa kiwango kinachotakiwa.

Wakati akihutubia, Rais Magufuli aliwaita hadharani Mkurugenzi wa Halmashauri, Mkandarasi na Naibu Waziri wa Tamisemi, ili watoe maelezo ni kwanini stendi kuu ya mkoa huo imechelewa kukamilika.

Akieleza sababu za kuchelewa kukamilisha kituo hicho cha mabasi, Naibu Waziri wa Tamisemi amesema tayari amezungumza na Mkandarasi mpya aliyekabidhiwa mradi huo na kusema kuwa mwisho wa mwezi huu utakuwa umekamilika na wamekubaliana kwamba endapo utakuwa bado watakana kwenye malipo yao.

Hivyo Rais baada ya kusikia hayo amewaomba wananchi wa mkoa huo kuwa wavumilivu kwa kipindi kilichobaki kusubiria kituo hiko cha mabasi kikamilike.

“Tumevulia tangu 2013.., siku 20 tutashindwa kuvumilia kweli ndugu zangu.., mimi nakuongeza siku 10 ziwe siku 30 kituo hicho kiwe kimekamilika.” Amesema Rais Magufuli.

Pia, Rais Magufuli ametoa onyo kali kwa wakandarasi wa ujenzi wa mradi huo wa stendi kuhakikisha ndani ya  kipindi tajwa kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa viwango vinavyotakiwa.

Young Killer alivyofuata nyayo za Gaddafi, ‘Utapigwa utachakaa’
CAG aanika upigaji mabilioni NHIF, NIC