Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameongeza siku 7 nyingine kwa Mkurugenzi wa Mashtaka DPP, Biswalo Mganga kuendelea kupokea barua kwa washtakiwa kesi ya uhujumu uchumi mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa washtakiwa 467 kukubali kutubu na kurejesha fedha walizohujumu.

Ambapo ndani ya siku 7 alizotoa mwanzo washtakiwa 467 wamekiri na kuahidi kurudisha jumla ya fedha bilioni 107 ambazo rais amesema zitatumika kwa matumizi mbalimbali kama vile kutengeneza barabara, kujenga hospitali pamoja na kulipa wafanyakazi.

Hata hivyo ametoa agizo kwa DPP kuwa wale wote watakaokamatwa kuanzia sasa sheria ichukue mkondo wake ili isijenge mazoea kwamba kesi ya uhumu uchumi si kesi.

”Niwaongezea siku 7, ila wale wote watakaoshikwa baada ya hizi siku 7 kwenye masuala ya uhujumu uchumi sheria ichukue mkondo wake isije sasa ikawa imejengeka mazeoa kwamba kesi ya uhujumu uchumi haipo, watakaoshikwa baada ya hizi siku saba, na wale ambao ni kesi mpya hausiki na huu msamaha”. Amesema Rais Magufuli.

Ameongezea kuwa siku saba alizotoa ni kwa wale ambao barua zao zimekwama gerezani na ameshauri DPP ahakiksihe anasimamia vyema suala hili kisheria ili washtakiwa waliotubu na kukiri waanze kuwa huru ili wakajumuike na familia zao na kuendelea na shughuli za kusaidia serikali katika kujenga taifa kwani anaamini kuwa biashara na shughuli walizokuwa wakifanya zimerudi nyuma.

Aidha ameongezea kuwa anafahamu wapo wanaodanganywa juu ya huu msamaha kuwa ni wa uongo amesisitiza kuwa hakuna msamaha wa uongo kwani ukishatoa msamaha ni msamaha na hawezi kutoa msamaha wa majaribio wala kumtega mtu.

”Ninafahamu wapo wengine wanadanganywa na mawakili wao, ili waendelee kupiga pesa, nimetoa hizi siku 7 nyingine, sitatoa tena” ameongezea Rais Magufuli.

Pia, Rais Magufuli ametoa wito kwa watanzania waliokuwa wana tuhuma za kuhujumu uchumi na wanania ya kutubu na kurudisha na kukiri wasiwe na wasiwasi kwamba ukishakiri kesho ndio ushahidi huo, Rais amesema hawezi kufanya kazi ya kitoto ya namna hiyo kwani ametoa msamaha na msamaha wake ni wa kweli.

Jambazi aliyesakwa muda mrefu auawa kwa risasi
Wahujumu uchumi 467 watubu, bilioni 107 kurudishwa