Hatimaye Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amewatuliza wanawake nchini humo baada ya kutangaza majina saba ya wanawake watakaokuwa sehemu ya baraza la mawaziri la nchi hiyo.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni wiki mbili baada ya Rais Kenyatta kutangaza majina ya mawaziri wapya bila kutaja jina la mwanamke hata mmoja.

Jumatatu, mamia ya wanawake waliandamana jijini Nairobi kupinga hatua hiyo ya Rais Kenyatta kutowaweka wanawake kwenye baraza hilo, hivyo kudai anavunja katiba ya nchi.

Kwa mujibu wa katiba ya Kenya, wanawake wanapaswa kuwa moja ya tatu ya jumla ya nafasi zote za uongozi Serikalini. Ingawa hatua hiyo haijafikiwa, Kenyatta ameonesha kuzingatia uwiano huo wa kijinsia hivyo baraza lake linakidhi vigezo kikatiba.

Rais Kenyatta ametangaza Baraza hilo la Mawaziri wakati ambapo Kambi ya NASA inaendelea na mipango yake ya kumuapisha aliyekuwa mgombea wake wa Urais, Raila Odinga.

Moto wateketeza wagonjwa hospitalini
Video: Makonda awamwagia sifa Walimu Jijini Dar