Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia ametoa pongezi kwa mwanamichezo daktari wa Sheria Dr.Damas Ndumbaro kwa kushinda kiti cha Ubunge Jimbo la Songea Mjini.

Rais Karia amesema ushindi wa Dr.Ndumbaro unaongeza wanamichezo zaidi katika bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanaweza kuwa chachu ya maendeleo ya michezo ikiwemo mpira wa miguu.

Amesema uzoefu wa Dr.Ndumbaro katika mpira wa miguu utasaidia katika nyanja hiyo na itasaidia kupaza sauti kupitia bunge katika harakati za kushirikiana kuusogeza mbele mchezo wa soka.

“Tunaamini uwezo wa Dr.Ndumbaro katika uongozi tumemuona katika mpira wa miguu akiongoza katika sehemu mbalimbali hakika uwezo wake wa uongozi ni mkubwa na atasaidia sana kukua kwa sekta hii ya michezo,sisi TFF tunamtakia kila la kheri kwenye majukumu yake mapya na tutampa ushirikiano wote kuhakikisha tunafikia mafanikio,kwetu ni faraja kubwa kuona wana familia wa mpira wa miguu wakishinda nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Ubunge”.Alisema Rais Karia.

Rais Karia ameongeza kuwa anaamini Dr.Ndumbaro jimbo lake la Songea Mjini litakuwa moja ya majimbo yenye mfano wa kuigwa katika maendeleo ya mpira wa miguu.

Dr.Ndumbaro amewahi kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwenye mpira wa miguu na hivi karibuni Rais Karia alimteuwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya rufaa ya leseni za klabu.

Akigombea kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dr.Ndumbaro amejizolea kura 45762 akiwazidi wagombea wengine 7 kutoka vyama mbalimbali.

Serengeti Boys kambini hadi Januari 28
Kamati ya nidhamu yamfungia Obrey Chirwa