Rais wa Ufilipino, Rodrigo Duterte ametishia kuwaua maofisa wa Jeshi la Polisi nchini humo (PNP) ambao wako chini ya uchunguzi wa makosa mbalimbali ya uhalifu.

Ametoa vitisho hivyo wakati akihutubia wananchi huku akiwalenga maafisa wa jeshi la polisi wanaoshirikiana na wahalifu.

Majina 102 ya maofisa wa polisi yaliyopelekwa kwa Duterte yako chini ya uchunguzi kwa makosa makubwa ya uhalifu yakiwemo ya ubakaji, kuteka, kupotosha na kujihusisha katika biashara ya dawa za kulevya.

“Maafisa hawa hawana maana na ni mzigo kwa jamii, maana wamekuwa wakifanya uhalifu na kushirikiana na wahalifu,”amesema Rais Durtete

Aidha, wengine wanalalamika kuwa uongozi huo unafanyakazi kizembe kama vile kutoka kazini bila idhini wala likizo na kushindwa kuhudhuria kwenye majukumu ya kimahakama.

Video: Rich Mavoko aishinda WCB ang'atuka rasmi
Harry Maguire, Jerome Boateng waigawa Man Utd

Comments

comments